Mungu anauita Mwili Wake wa kimataifa kuwafanya watoto kuwa kipaumbele… Sio tu kuwafikia, bali kuwatia nguvu na kuwaona kama viongozi na waanzilishi katika kutimiza Agizo Kuu.
Ono la 2BC ni kuona watoto kila mahali wakisikia sauti ya Baba yao wa Mbinguni, wakijua utambulisho wao katika Kristo na kutiwa nguvu na Roho wa Mungu kushiriki upendo Wake!
Harakati za maombi na utume za kimataifa na kikanda zinakumbatia maono ya 2BC duniani kote ikiwa ni pamoja na International Prayer Connect, GO Movement, Billion Soul Harvest, Transform World, 4 to 14 Window, Global 2033, Finishing the Task, Great Commission Coalition na nyinginezo. Timu ya uongozi inayowakilisha Asia, Afrika, Ulaya na Amerika imeanzishwa.